• HABARI MPYA

  Friday, April 01, 2022

  POLISI YALAZIMISHWA SARE, 1-1 NA RUVU


  WENYEJI, Polisi Tanzania wamelazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Tariq Seif alianza kuifungia Polisi dakika ya sita, kabla ya Samson Joseph kuisawazishia Ruvu Shooting dakika ya 83.
  Kwa matokeo hayo, Polisi inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 18 na kusogea nafasi ya saba, wakati Ruvu inafikisha pointi 21 katika mchezo wa 29 na kusogea nafasi ya 10.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI YALAZIMISHWA SARE, 1-1 NA RUVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top