• HABARI MPYA

  Sunday, August 15, 2021

  YANGA SC WALIVYOONDOKA KWENDA MOROCCO KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA MSIMU MPYA


  KIKOSI cha Yanga kimeondoka leo kwenda Morocco kuweka kambi ya kujiandaa na msimu hadi itakaporejea kwa ajili ya tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 29.
  Yanga imeondoka baada ya kutambulisha wachezaji wapya tisa, ambao ni makipa Eric Johola (Aigle Noir), Djigui Diarra (Stade Malien), beki wa kushoto, David Bryson (KMC ) na beki wa kulia Djuma Shabani (AS Vita).
  Wengine ni winga wa kulia, Jesus Moloko (AS Vita), winga wa kushoto, Dickson Ambundo (Dodoma Jiji FC), washambuliaji Yussuf Athumani (Biashara United), Fiston Mayele (AS Vita) na Heritier Makambo (Horoya).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WALIVYOONDOKA KWENDA MOROCCO KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA MSIMU MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top