• HABARI MPYA

  Wednesday, August 11, 2021

  AZAM FC YATUPWA NJE KWA MATUTA NA BIG BULLET YA MALAWI NUSU FAINALI YA KOMBE LA KAGAME LEO CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wametupwa nje ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya kuchapwa kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 2-2 na Big Bullet ya Malawi usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Sasa Big Bullet itakutana na Express ya Uganda katika fainali Jumamosi, timu zote zilikuwa Kundi A pamoja na Yanga na Atalabara ya Sudan Kusini.
  Na Azam FC itawania nafasi ya tatu dhidi ya KMKM ya Zanzibar, timu ambazo zililuwa pamoja Kundi B na KCCA ya Uganda na Le Messager Ngozi ya Burundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATUPWA NJE KWA MATUTA NA BIG BULLET YA MALAWI NUSU FAINALI YA KOMBE LA KAGAME LEO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top