• HABARI MPYA

  Thursday, August 26, 2021

  BAYERN WASHINDA 12-0 KOMBE LA UJERUMANI

  MABINGWA wa Ujerumani, Bayern Munich usiku wa Jumatano wameionea timu ya daraja la Tano nchini humo, Bremer SV baada ya kuichapa mabao 12-0 katika mchezo wa Raundi ya Kwanza Kombe la Ujerumani Uwanja wa Wohninvest Weser mjini Bremen.
  Katika mchezo huo ambao kocha Julian Nagelsmann aliwapumzisha nyota wake tegemeo kabisa, Robert Lewandowski, Leon Goretzka na Manuel Neuer mabao ya Bayern Munich yamefungwa na Eric Maxim Choupo Moting manne, Jamal Musiala mawili, Malik Tillman, Leroy Sane, Jan-Luca Warm aliyejifunga, Michael Cuisance, Bouna Sarr na Corentin Tolisso kila mmoja moja.
  Ushindi mkubwa zaidi kihistoria kwa Bayern Munich ni 23-0 katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu dhidi ya FC Rottach Egern mwaka 2019. 
  Vigogo hao wa Ujerumani waliichapa timu hiyo hiyo mabao 20-2 mwaka uliotangulia.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYERN WASHINDA 12-0 KOMBE LA UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top