• HABARI MPYA

  Tuesday, August 24, 2021

  YANGA SC KUMENYANA NA ZANACO JUMAPILI DAR  VIGOGO, Yanga SC watamenyana na Zanaco ya Zambia katika mchezo wa kirafiki kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam 
  Siku hiyo pia mwanamuziki nguli barani Afrika, Koffi Olomide atatumbuisha kwenye tamasha hilo maalum kwa Yanga kuzindua rasmi msimu mpya kwa kutangaza kikosi chake pamoja na jezi itakazotumia nyumbani na ugenini msimu ujao..
  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Suma Mwaitenda alisema jana pamoja na Koffi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) watakuwepo wasanii wengine mbalimbali wa nyumbani.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC KUMENYANA NA ZANACO JUMAPILI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top