• HABARI MPYA

  Saturday, August 07, 2021

  KMKM NAYO YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUICHAPA AZAM FC 3-2 LEO, KCCA YATUPWA NJE

  KMKM ya Zanzibar imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya wenyeji, Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Nusu Fainali zitachezwa Jumatatu na KMKM iliyomaliza nafasi ya pili Kundi B, itamenyana na Express ya Uganda iliyoongoza Kundi A, wakati Azam FC iliyoongoza Kundi B itakutana na Nyasa Big Bullet iliyoshika nafasi ya pili Kundi B.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMKM NAYO YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUICHAPA AZAM FC 3-2 LEO, KCCA YATUPWA NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top