• HABARI MPYA

  Saturday, August 14, 2021

  AZAM FC YAZINDUA NEMBO MPYA LEO HOTELI YA SERENA KATIKA SHUGHULI ILIYOHUDHURIWA NA WAZIRI WA MICHEZO NA VIONGOZI WA TFF

   KLABU ya Azam FC leo imezindua nembo mpya itakayoanza kutumika mara moja na kuachana na ya zamani iliyokuwa inatumika tangu kuanzishwa kwa timu mwaka 2004.
  Zoezi hilo limefanyika leo katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.
  Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdukarim Amin 'Popat' amesema kwamba nembo ni kitu muhimu katika utambulisho wa taasisi yoyote.
  "Inavutia watu kukufuatilia kwa umakini na kwa ukaribu zaidi. Husaidia kutengeneza ushawishi wa haraka kwa mtu anayeiona kwa mara kwanza. Ni msingi mkuu wa utambulisho wa jina chapa,".


  "Huitenganisha taasisi na washindani wake kibiashara. Hutengeneza uaminifu wa chapa kwa wafuasi wake," amesema.
  Popat amesema Azam kama klabu wamezingatia yote hayo katika kufikia maamuzi ya kuja na nembo hiyo mpya.
  "Wakati tukiwa katika mradi mpya kuelekea msimu mpya na misimu mingine mbele, ni matarajio yetu nembi hii itatusadia kutujengea taswira mpya na matumaini mapya," ameongeza Popat.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAZINDUA NEMBO MPYA LEO HOTELI YA SERENA KATIKA SHUGHULI ILIYOHUDHURIWA NA WAZIRI WA MICHEZO NA VIONGOZI WA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top