• HABARI MPYA

  Wednesday, August 18, 2021

  SIMBA SC YAMSAJILI WINGA WA GWAMBINA


  MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamemtambulisha winga chipukizi, Jimson Steven Mwanuke mwenye umri wa muaka 18 kuwa mchezaji wao mpya kuelekea msimu ujao.

  Huyo anakuwa mchezaji mpya wa nane baada ya kiungo mkabaji, Abdulsamad Kassim Ali ' Guti' kutoka Kagera Sugar ya Bukoba na beki wa kulia, Israel Patrick Mwenda kutoka KMC ya Kinondoni.

  Wengine ni beki wa kati Mkongo Henoc Inonga Baka kutoka DC Motema Pembe ya kwao, Kinshasa, mawinga Msenegal, Msenegal Papa Ousmane Sakho kutoka Teungueth Rufisque ya kwao na Yussuf Mhilu kutoka Kagera Sugar ya Bukoba.

  Wengine ni Wamalawi, Peter Banda kutoka Nyasa Big Bullet ya kwao, Blantyre na kiungo Duncan Nyoni kutoka Silver Strikers ya kwao, Lilongwe na wote wapo kambini Jijini Rabat nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya.

  Ikumbukee msimu ujao Simba itawakosa nyota wake wawili walioibeba timu kwa misimu miwili iliyopita, winga wa Msumbiji Luis Miquissone aliyeuzwa Al Ahly ya Misri na kiungo Mzambia, Clatous Chama aliyeuzwa RSB Berkane ya Morocco.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMSAJILI WINGA WA GWAMBINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top