• HABARI MPYA

  Monday, August 16, 2021

  GWIJI WA SOKA UJERUMANI, GERD MULLER AFARIKI DUNIA

  GWIJI wa soka Ujerumani, Gerd Muller, mshambuliaji aliyeifungia Ujerumani Mgharibi goli la ushindi katika Kombe la Dunia mwaka 1974 amefariki dunia jana akiwa ana umri wa miaka 75 baada ya miaka sita ya kusumbuliwa maradhi ya Azeima, ugonjwa wa ubongo ambao mara nyingi huwapata wazee.
  Muller mmoja wa wachezaji bora wa kizazi chake pia aliisaidia West Germany kushinda mataji ya Euro 1972 na akashinda mataji matatu ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Bayern Munich.
  Katika miaka yake miaka 15 Bayern, Muller ameweka rekodi ya kufunga mabao 365 katika mechi 427 Bundesliga na mengine 66 katika mechi 74 za michuano ya Ulaya.


  Mshambuliaji wa sasa wa Bayern, Robert Lewandowski alifanikiwa kuvunja rekodi ya Muller dakika ya mwisho katika mechi ya mwisho msimu uliopita ambayo imedumu tangu msimu wa 1971-72 alipofunga mabao 40 msimu mmoja.
  Lewandowski alifunga bao la 41 dakika ya 90 kukamilisha ushindi wa 5-2 dhidi ya Augsburg katika Raundi ya mwisho ya Ligi ya Ujerumani mwezi Mei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GWIJI WA SOKA UJERUMANI, GERD MULLER AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top