• HABARI MPYA

  Saturday, August 14, 2021

  KMKM YAIPIGA AZAM FC PUNGUFU 1-0 NA KUTWAA NAFASI YA TATU KOMBE LA KAGAME LEO MKAPA


  KMKM ya Zanzibar imefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu kwenye michuano ya Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo ambao Azam FC ilimaliza pungufu baada ya mchezaji wake, Oscar Masai kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 76, bao pekee la KMKM limefungwa na Ilyasa Mohamed dakika ya tatu tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMKM YAIPIGA AZAM FC PUNGUFU 1-0 NA KUTWAA NAFASI YA TATU KOMBE LA KAGAME LEO MKAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top