• HABARI MPYA

  Thursday, August 26, 2021

  SAKHO AFUNGA TENA SIMBA SC YATOA SARE 1-1 MOROCCO

   MABINGWA wa Tanzania, Simba SC leo wametoa sare ya 1-1 na wenyeji, Khourigba katika mchezo wa kirafiki mjini Rabat nchini Morocco.
  Kiungo Papa Ousmane Sakho alianza kuifungia Simba dakika ya 37, kabla ya Mseegal mwenzake, mshambuliaji Adama Diom kuisawizishia Khourigba dakika ya 61.
  Huo unakuwa mchezo wa pili katika kambi ya Simba ya kujiandaa na msimu mpya mjini humo kufuatia sare nyingine, 2-2 na FAR Rabat wiki iliyopita.


  Mabao ya Simba siku hiyo yalifungwa na viungo Hassan Dilunga dakika ya 54 na Sakho dakika ya 81 baada ya FAR Rabat kutangulia kwa mabao ya Chabani dakika ya 14 na Abba dakika ya 26.
  Simba SC imeweka kambi Rabat kwa wiki ya pili sasa ikijiandaa na msimu mpya, lengo lao kuendeleza mafanikio yao yaliyodumu kwa misimu minne iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAKHO AFUNGA TENA SIMBA SC YATOA SARE 1-1 MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top