• HABARI MPYA

  Saturday, August 14, 2021

  SIMBA SC YASAJILI WINGA HATARI WA KUSHOTO MSENEGAL KUTOKA KLABU YA TEUNGUETH YA KWAO


  KLABU ya Simba imemtambulisha winga wa kushoto Msenegal, Papa Ousmane Sakho mwenye umri wa miaka 24 kutoka Teungueth Rufisque ya kwao kuwa mchezaji wake mpya wa nne kuelekea msimu ujao.
  Sakho anakuwa mchezaji mpya wa nne dirisha hili baada ya mawinga wengine, mzawa Yussuf Mhilu kutoka Kagera Sugar ya Bukoba na Mmalawi, Peter Banda kutoka Nyasa Big Bullet ya kwao, Blantyre.
  Simba SC ambayo tayari ipo kambini nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya pia imemsajili kiungo Mmalawi, Duncan Nyoni kutoka Silver Strikers ya kwao, Lilongwe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI WINGA HATARI WA KUSHOTO MSENEGAL KUTOKA KLABU YA TEUNGUETH YA KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top