• HABARI MPYA

  Thursday, August 12, 2021

  LUKAKU AREJEA CHELSEA KWA DAU LA PAUNI MILIONI 98


  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ubelgiji, Romelu Lukaku akikabidhiwa jezi ya Chelsea na Mkurugenzi, Marina Granovskaia kufuatia kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 98 kurejea The Blues kutoka Inter Milan.
  Lukaku, mwenye umri wa miaka 28 sasa, anarejea Chelsea baada ya kushindwa kung’ara awali alipojiunga na timu hiyo akiwa ana umri wa miaka 18 tu kutoka Anderlecht ya kwao, Ubelgiji. 


  Hata hivyo, baada ya misimu mitatu Stamford Bridge akicheza mechi 15 tu akatimkia Everton na baada ya hapo akafanikiwa kufanya vizuri na kuingia kwenye orodha ya washambuliaji tishio Ulaya.
  Lukaku alifunga mabao 87 katika mechi 166 Everton, akafunga mengine 42 katika mechi 96 Manchester United na 64 katika mechi 95 Inter. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AREJEA CHELSEA KWA DAU LA PAUNI MILIONI 98 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top