• HABARI MPYA

  Friday, August 20, 2021

  YANGA SC YATAMBULISHA MKONGO MWINGINE  HATIMAYE klabu ya Yanga imemtambulisha beki wake mpya, Mkongo, Yannick Bangala Litombo kutoka FAR Rabat ya Morocco.
  Beki huyo wa zamani wa AS Vita ya kwao, Kinshasa anakuwa mchezaji mpya wa 11 Yanga SC baada ya Wakongo wenzake, beki Djuma Shabani AS Vita, winga Jesus Moloko na washambuliaji Fiston Mayele wote kutoka AS Vita na Heritier Makambo kutoka Horoya ya Guinea.
  Wengine wapya ni makipa Eric Johola kutoka Aigle Noir ya Burundi, Djigui Diarra kutola Stade Malien ya kwao, Mali, beki David Bryson kutoka KMC ya Kinondoni, viungo, Khalid Aucho (Misr Lel Makkasa SC), Dickson Ambundo kutoka Dodoma Jiji FC na mshambuliaji Yussuf Athumani kutoka Biashara United.
  Yanga imeweka kambi Jijini Marrakech nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya ambao watauzindua Agosti 29 kwenye tamasha la Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATAMBULISHA MKONGO MWINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top