• HABARI MPYA

  Sunday, August 15, 2021

  PSG YAMTAMBULISHA MESSI KABLA YA KUICHAPA STRASBOURG 4-2

  KLABU ya Paris Saint-Germain ilimtambulisha mchezjai wake mpya, Lionel Messi mbele ya mashabiki Uwanja wa Parc des Princes kabla ya mchezo wao wa kwanza wa  Ligue 1 wakiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Strasbourg.
  Messi alirudi jukwaani kushuhudia mabao ya Mauro Icardi dakika ya tatu, Kyllian. Mbappé dakika ya 25, Julian Draxler dakika ya 27 na Pablo Sarabia dakika ya 86 yakiing’arisha PSG.  
  Messi mwenye umri wa miaka 34 amesaini mkataba wa miaka miwili PSG baada ya miaka 20 ya kuichezea Barcelona akianzia timu ya vijana mwaka 2000 na jumla amecheza mechi 778, amefunga mabao 672 na kuiwezesha kushinda mataji 35, yakiwemo 10 ya La Liga na manne ya Champions League.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PSG YAMTAMBULISHA MESSI KABLA YA KUICHAPA STRASBOURG 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top