• HABARI MPYA

  Sunday, August 29, 2021

  YANGA SC WACHAPWA 2-1 NA ZANACO DAR  WENYEJI, Yanga SC wamechapwa 2-1 na Zanaco ya Zambia katika mchezo wa kirafiki kuhitimisha tamasha la kilele cha Wiki ya Mwananchi usiku wa leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar sa Salaam.
  Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Heritier Makambo alianza kuifungia Yanga dakika ya 30 baada ya kuwachambua mabeki wawili wa Zanaco kufuatia pasi ya kiungo mzawa, Feisal Salum na kufumua shuti lililojaa nyavuni.
  Winga wa kulia Ackim Mumba akaisawazishia Zanaco dakika ya 60, kabla ya kiungo Kelvin Kapumbu kufunga la ushindi dakika ya 76 na kuzima kabisa shangwe za maelfu ya mashabiki wa Yanga waliofurika Uwanja wa Mkapa leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WACHAPWA 2-1 NA ZANACO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top