• HABARI MPYA

  Tuesday, August 10, 2021

  AGUREO HATOANZA KUICHEZEA BARCELONA HADI OKTOBA

  MSHAMBULIAJI mpya, Muargentina Sergio Aguero hataanza kuitumikia Barcelona hadi katikati ya Oktoba kutokana na maumivu ya nyuma ya mguu, kigimbi, kitaalamu calf.
  Barcelona, ambayo tayari nyota wake mwingine, Muargentina, Lionel Messi anaondoka ilitoa taarifa hiyo baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Juventus kwenye mchezo wa kirafiki juzi.
  Aguero mwenye umri wa miaka 33 alisajiliwa Julai kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba Manchester City, ambako alikuwa anasumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara.

  Lakini pamoja na maumivu ya mara kwa marah katika misimu yake yote 10 aliyoichezea City bado Aguero ameondoka Etihad na rekodi ya ufungaji bora wa muda wote kwa mabao yake 260.
  Amesaini mkataba wa hadi mwishoni mwa msimu wa 2022-23 kwa dola za Kimarekani Milioni 117.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AGUREO HATOANZA KUICHEZEA BARCELONA HADI OKTOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top