• HABARI MPYA

  Wednesday, August 11, 2021

  BIASHARA UNITED YASAJILI MSHAMBULIAJI MKENYA NA WENGINE WAZAWA WAWILI KUIMARISHA KIKOSI CHAKE

   

  KATIKA kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao, wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Biashara United ya Mara imemsajili mshambuliaji Mkenya, Tayo Odongo Mathew kutoka Zoo FC ya kwao.
  Pamoja na huyo imemsajili mshambuliaji wa zamani wa Njombe Mji FC, Notikeli John Masasi na Anicet Revocatus Kezilahabi kutoka Mwadui FC wanaoungana na mshambuliaji Atuepele Green Jackson kutoka Geita Gold kufanya idadi ya wachezaji wapya wanne hadi sasa.
  Ikumbukwe Biashara United imeacha wachezaji 14, mbali ya wale ambao wanaondoka akiwemo Yussuf Athumani aliyejiunga na Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YASAJILI MSHAMBULIAJI MKENYA NA WENGINE WAZAWA WAWILI KUIMARISHA KIKOSI CHAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top