• HABARI MPYA

  Wednesday, August 11, 2021

  RASMI, MESSI NI MCHEZAJI MPYA WA PSG KWA MIAKA MIWILI IJAYO

  HATIMAYE nyota Muargentina, Lionel Messi amekamilisha uhamisho wake Paris Saint-Germain kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Barcelona.
  Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, amesaini mkataba wa miaka miwili na atakuwa analipwa mshahara wa Pauni Milioni 1 kwa wiki, sawa na Pauni Miliono 35 kwa mwaka.
  Mshindi huyo wa Ballon d'Or sita anakwenda Parc des Princes kukutana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona, Mbrazil Neymar Jijini Paris na mshambuliaji mwingine nyota, Mfaransa, Kylian Mbappe.


  Messi ameshinda mataji 35 Barcelona alikodumu kwa miaka 21  tangu awasili akiwa na umri wa miaka 15 na akacheza mechi yake ya kwanza timu ya wakubwa mwaka 2004 alipofikisha miaka 16. 
  Kwa ujumla amecheza mechi 778 na kuweka rekodi ya mfungaji bora wa muda wote kwa mabao yake 672, yakiwemo 120 ya kwenye Ligi ya Mabingwa na 474 ya rekodi kwenye LaLiga.    
  Pia ameshinda mataji 10 ya LaLiga, manne ya Ligi ya Mabingwa na saba ya Kombe la Mfalme.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RASMI, MESSI NI MCHEZAJI MPYA WA PSG KWA MIAKA MIWILI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top