Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea alizaliwa Brazil, lakini hajawi kucheza nyumbani kwao, kwani kisoka aliibukia Braga ya Ureno mwaka 2006 na akajipatia umaarufu alipokwenda Madrid kati ya 2010-2014 kabla ya kwenda Chelsea na kurejea Hispania mwaka 2018.
Ni mshindi wa mataji mawili ya La Liga na moja la Ligi Kuu ya England pamoja na Europa League aliloshinda na Atletico Madrid mwaka 2018.
Costa aliyeichezea Hispania katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 na 2018, ameifungia mabao 10 katika mechi 24 timu yake hiyo ya taifa.
Huko anaungana na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Hulk na kwa ‘mziki’ wake, Atletico Mineiro ni moja ya timu inayopewa nafasi kubwa kutwaa Copa Libertadores msimu huu.
0 comments:
Post a Comment