// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA QUEENS YATOA SARE NA WAGANDA CECAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA QUEENS YATOA SARE NA WAGANDA CECAFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Tuesday, August 31, 2021

  SIMBA QUEENS YATOA SARE NA WAGANDA CECAFA

  TIMU ya Simba Queens leo imetoka sare ya 0-0 na Lady Doves WFC ya Uganda Uwanja wa Moi Kasarani Jijini Nairobi nchini Kenya katika mchezo wake wa pili wa Kundi A kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake ukanda wa Afrika Mashariki.
  Kwa matokeo hayo, Queens inafikisha pointi nne kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya PVP FC ya Burundi kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi Uwanja wa Nyayo, Nairobi na watakamilisha mechi za kundi lao Ijumaa kwa kumenyana na FAD FC ya Djibouti.
  Bingwa atashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu nchini Misri, ambayo itahusisha timu nane, nyingine kutoka kanda nyingine barani zitakazogawanywa katika makundi mawili.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YATOA SARE NA WAGANDA CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top