• HABARI MPYA

  Saturday, August 21, 2021

  KIDUKU AMPIGA TENA DULLAH, AZAWADIWA GARI

  BONDIA Twaha Kassim Rubaha ‘Twaha Kiduku’ ameendeleza ubabe kwa rafiki yake, Abdallah Shaaban Pazi ‘Dullah Mbabe' baada ya kumshinda kwa pointi usiku huu ukumbi wa Ubungo Plazza Jijini Dar es Salaam.
  Kiduku alianza vibaya pambano hilo baada ya kuangushwa raundi ya kwanza tu, lakini akainuka na kumalizia raundi baada ya kuhesabiwa na refa.
  Kutoka hapo Kiduku alitawala pambano kwa raundi zote tisa zilizofuatia na majaji wote wakampa ushindi wa pointi 98-91. wamepima uzito leo tayari kwa pambano lao kesho ukumbi wa Ubungo Plazza, Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, pamoja na malipo ya kawaida lakini Kiduku amekabidhiwa gari aina ya Toyota Crown Athlete. Hilo lilikuwa pambano la tatu baina yao kufuatia kutoka droo Oktoba 21, mwaka 2017 ukumbi wa Msasani Club kabla ya Kiduku kushinda kwa pointi Agosti 28, mwaka jana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  GONGA HAPA KUTAZAMA VIDEO

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIDUKU AMPIGA TENA DULLAH, AZAWADIWA GARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top