• HABARI MPYA

    Saturday, August 14, 2021

    AZAM TV YAWAONYA TV ZA MITANDAONI, CABLE KUTORUSHA MECHI ZA LIGI KUU, ASFC BILA RUHUSA YAO

     TAARIFA KWA UMMA

    HAKI YA KURUSHA MATANGAZO MBASHARA YA LIGI KUU TANZANIA BARA, LIGI KUU UJERUMANI (BUNDESLIGA), KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM (ASFC), MECHI ZOTE ZA TIMU YA TAIFA ‘TAIFA STARS’, MASHINDANO YA KLABU ZA AZAM FC, SIMBA NA YANGA PAMOJA NA MAPAMBANO YA NGUMI (VITASA) MSIMU WA 2021/2022 NDANI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    AZAM MEDIA LIMITED (AML), ni kampuni ya habari ambayo imejikita katika utoaji wa habari za maudhui mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mashindano mbalimbali ya michezo hasa mpira wa miguu, mbio za magari, mapambano ya ngumi na michezo mingine. AML imejikita pia katika kukuza fani ya sanaa na hasa kuwaendeleza wazalishaji wa ndani wanaojishughulisha na sinema na tamthilia za ndani ya nchi. AML imekuwa pia ikionyesha tamthilia kutoka nje ya nchi ambazo nyingi zimekuwa zikitafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ili kuwafanya Watanzania wengi kuelewa na kupata burudani na kutimiza ahadi yetu ya ‘Burudani kwa Wote’. Huduma za matangazo hayo zimekuwa zikifanyika ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadhi ya nchi katika bara la Afrika.

    AML inapenda kuwafahamisha wamiliki wa mitandao ya kijamii, wamiliki wa mitandao ya kurusha matangazo kwa njia ya waya (cable)makampuni mengine ya utangazaji na umma kwa ujumla kuwa AZAM MEDIA LIMITED (AML)imepewa haki zote za kurusha matangazo ya mashindano yafuatayo:

    1. LIGI KUU TANZANIA BARA
    2. KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM (ASFC)
    3. MECHI ZOTE ZA TAIFA STARS
    4. MASHINDANO MENGINE YA KLABU YA AZAM FC
    5. MASHINDANO MENGINE YA KLABU YA SIMBA
    6. MASHINDANO MENGINE YA KLABU YA YANGA
    7. LIGI KUU YA UJERUMANI (BUNDESLIGA)
    8. NGAO YA JAMII (NGAO YA HISANI)
    9. MAPAMBANO YA NGUMI (VITASA

    Matangazo ya mashindano haya hurushwa kupitia chaneli mbalimbali za AZAM TV zinazopatikana katika king’amuzi cha AZAM. Haki za kurusha matangazo haya ni kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nchi nyingine za Afrika ambako kuna visimbuzi vya AZAM.

    Kwa maana hiyo hakuna chombo kingine cha habari yaani televisheni, mitandao ya kijamii au cable inayoruhusiwa kurusha matangazo hayo bila makubaliano maalumu na AZAM MEDIA LIMITED. Kwenda kinyume na matakwa hayo itakuwa ni kinyume cha sheria, kanuni na makubaliano ya hakimiliki. 

    AZAM MEDIA LIMITED (AML), haitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayekwenda kinyume na utaratibu huo. Tutashirikiana na mamlaka husika kupambana na wote watakaoonyesha matangazo hayo bila idhini ya AZAM MEDIA LIMITED.

     

     

    Imetolewa na:

    AZAM MEDIA LIMITED (AML)

    Agosti 122021



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM TV YAWAONYA TV ZA MITANDAONI, CABLE KUTORUSHA MECHI ZA LIGI KUU, ASFC BILA RUHUSA YAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top