• HABARI MPYA

  Wednesday, August 25, 2021

  UKAGUZI KIRUMBA KWA AJILI YA KOMBE LA AFRIKA

  MENEJA wa Leseni za Klabu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jonas Kiwia akifanya ukaguzi Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kama unakidhi vigezo vya kutumika kwa mechi za nyumbani za Biashara United ya Mara kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
  Katika ukaguzi huo, Kiwia aliambatana na Mtendaji Mkuu wa Biashara United, Haji Matete, Katibu wa Chama cha Soka Mwanza (MZFA), Leonard Malongo na Katibu wake Msaidizi, Khalid Bitebo.
  Biashara United itaanzia ugenini dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti kati ya Septemba 10 na 12 kabla ya kurejea nyumbani kwa mechi ya marudiano ya kati ya Septemba 17 na 19 na ikivuka hapo itakutana na mshindi kati ya Hay Alwady Nyala ya Sudan na Al Ahli Tirpoli ya Libya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UKAGUZI KIRUMBA KWA AJILI YA KOMBE LA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top