• HABARI MPYA

  Monday, August 30, 2021

  COASTAL UNION YAPATA KOCHA MMAREKANI

   KLABU ya Coastal Union ya Tanga imeingia mkataba wa miaka miwili na Kocha Mmarekani, Melis Medo kuinoa timu hiyo.
  Medo anachukua nafasi ya Juma Mgunda ambaye sasa anakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 1988.
  Taarifa ya Coastal Union imesema kwamba aliyekuwa msaidizi wa Mgunda, Joseph Lazaro ataendelea kuwa Kocha Msaidizi wa Medo.
  Medo alikuwa Kocha wa Gwambina kuanzia Mei mwaka huu baada ya kufundisha klabu kadhaa nchini Kenya ikiwemo Wazito na Sofapaka.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAPATA KOCHA MMAREKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top