• HABARI MPYA

  Saturday, August 21, 2021

  SIMBA YATOA SARE YA 2-2 NA FAR RABAT MOROCCO

  MABINGWA wa Tanzania, Simba SC leo wametoa sare ya 2-2 na wenyeji, FAR Rabat katika mchezo wa kirafiki leo Jijini Rabat nchini Morocco.
  Mabao ya Simba yamefungwa na viungo Hassan Dilunga dakika ya 54 na Papa Msenegal Ousmane Sakho dakika ya 81 baada ya FAR Rabat kutangulia kwa mabao ya Mohsinne Abba dakika ya 14 na ya 26.
  Simba SC imeweka kambi Rabat kwa zaidi ya wiki sasa ikijiandaa na msimu mpya, lengo lao kuendeleza mafanikio yao yaliyodumu kwa misimu minne iliyopita.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YATOA SARE YA 2-2 NA FAR RABAT MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top