• HABARI MPYA

  Friday, August 13, 2021

  RAIS WA CAF, BILIONEA PATRICE MOTSEPE AKUTANA NA WAZIRI MKUU MHESHIMIWA MAJALIWA KWA MAZUNGUMZO DODOMA


  WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo amekutana kwa mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Bilionea Patrice Motsepe ofisini kwake Mlimwa Jijini Dodoma.
  Motsepe, raia wa Afrika Kusini na mmiliki wa klabu ya Mamelodi Sundowns yupo nchini kwa mwaliko wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na kesho atahudhuria fainali ya Kombe la Kagame kati ya Express ya Uganda na Nyasa Big Bullet ya Malawi Dar es Salaam.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS WA CAF, BILIONEA PATRICE MOTSEPE AKUTANA NA WAZIRI MKUU MHESHIMIWA MAJALIWA KWA MAZUNGUMZO DODOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top