• HABARI MPYA

  Tuesday, August 10, 2021

  EXPRESS YA UGANDA YATINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUICHAPA KMKM YA ZA ZANZIBAR 2-1 USIKU HUU CHAMAZI


  TIMU ya Express ya Uganda imefanikiwa kwenda Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya KMKM ya Zanzibar leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Express yamefungwa na Muzamil Mutyaba dakika ya 56 na Eric Kambale dakika ya 90, wakati la KMKM limefungwa na Ibrahim Abdallah dakika ya 45.
  Sasa Tai Wekundu wa Kampala watakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho baina ya wenyeji, Azam FC na Nyasa Big Bullet ya Malawi hapo hapo Chamazi na fainali itafanyika Jumamosi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EXPRESS YA UGANDA YATINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME BAADA YA KUICHAPA KMKM YA ZA ZANZIBAR 2-1 USIKU HUU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top