• HABARI MPYA

  Wednesday, August 18, 2021

  RATIBA YA KRISIMASI NBA, BUCKS KUWA NYUMBANI

  RATIBA ya mechi za Krisimasi za NBA imetoka na mabingwa watetezi, Milwaukee Bucks watakuwa nyumbani dhidi ya Boston Celtics.
  Mechi nyingine siku hiyo, Atlanta Hawaks watamenyana na New York Knicks, Golden State Warriors watawafuata mabingwa wa Western Conference, Phoenix Suns.
  Nao Brooklyn Nets watacheza na Los Angeles Lakers, wakati Denver Nuggets watakwenda kwa Utah Jazz katika mechi ya mwisho siku hiyo.
  Ratiba kamili ya msimu mpya NBA itatoka Ijumaa mchana, huku Jumamosi ligi ikirejea kwenye mechi 82 kwa msimu baada ya mechi 72 msimu uliopita kwa sababu ya janga la COVID 19.
  Aidha, pia inatarajiwa Toronto Raptors – ambao msimu uliopita walichezea mechi zao Tampa, Florida – wataruhusiwa kucheza nyumbani kwao, Canada msimu huu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RATIBA YA KRISIMASI NBA, BUCKS KUWA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top