• HABARI MPYA

  Saturday, August 28, 2021

  TORRES APIGA MBILI MAN CITY YAICHAPA ARSENAL 5-0


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameendeleza 'mauaji' baada ya kuichapa Arsenal 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad, Manchester huo ukiwa ushindi wa pili katika mechi tatu, kufuatia kuchapwa 1-0 na Tottenham Hotspur na kushinda 5-0 dhidi ya Norwich City. 
  Katika mchezo huo ambao Arsenal ilimaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Granit Xhaka kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 35 kwa kumchezea rafu Joao Cancelo, mabao ya Man City yamefungwa na Ilkay Gundogan dakika ya saba, Ferran Torres dakika ya 12 na 84, Gabriel Jesus dakika ya 43 na Rodri dakika ya 53.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TORRES APIGA MBILI MAN CITY YAICHAPA ARSENAL 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top