• HABARI MPYA

  Thursday, August 12, 2021

  KIUNGO ALIYEWAHI KUCHEZA YANGA, MTIBWA SUGAR, KAGERA SUGAR NA MBEYA CITY AFARIKI DUNIA LEO ARUSHA

  KIUNGO Babu Ally Seif (28) aliyewahi kuchezea Yanga kwa muda mfupi mwaka 2017 amefariki dunia leo Jijini Arusha baada ya kuugua kwa muda mfupi.
  Taarifa zinasema Babu alikuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu na baada ya hali yake kubadilika ghafla leo alipelekwa hospitali ambako umauti ulimkuta.
  Babu Ally aliyechezea Yanga Juni 2017 kwenye michuano ya SportPesa Super Cup chini ya kocha Juma Mwambusi na Nsajigwa Shadrack baada ya Mzambia George Lwandamina kuondoka - lakini akaondoka baada ya mashindano hayo kwenda Mbeya City.


  Kisoka aliibukia Morani FC ya Arusha mwaka 2010 kabla ya kwenda Mtibwa Sugar mwaka 2011 ambako alicheza hadi 2013 akaenda JKT Oljoro ya Arusha, 2014 Kagera Sugar hadi 2017 Mbeya City na mara ya mwisho alichezea Lipuli FC hadi inashuka daraja 2019.
  Mungu ampumzishe kwa amani Babu Ally Seif aliyezaliwa Desemba 15, mwaka 1993.

  Babu Ally Seif amewahi pia kuchezea timu ya taifa mwaka 2012na 2014
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIUNGO ALIYEWAHI KUCHEZA YANGA, MTIBWA SUGAR, KAGERA SUGAR NA MBEYA CITY AFARIKI DUNIA LEO ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top