• HABARI MPYA

  Tuesday, August 17, 2021

  TFF YATANGAZA TENDA NGAO YA JAMII


  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza tenda ya kurusha matangazo moja kwa moja mechi ya Ngao ya Jamii baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga mwezi ujao.
  Mechi hiyo ya kuashiria upenuzi wa pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022 itachezwa Jumamosi ya Septemba 25, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mechi ya Ngao ya Jamii hukutanisha bingwa wa Ligi Kuu ya na Mshindi wa Kombe la TFF, maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), mataji ambayo yote yalichukuliwa na Simba msimu uliopita.
  Lakini kwa sababu Yanga ndio waliomaliza nafasi ya pili Ligi Kuu pia ndio walicheza na Simba fainali ya ASFC Julai 25 na kufungwa 1-0 mjini Kigoma ndio maana watawania Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YATANGAZA TENDA NGAO YA JAMII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top