• HABARI MPYA

  Monday, August 23, 2021

  PRISONS YASAJILI KIPA WA AZAM, MSHAMBULIAJI WA SIMBA SC

  KATIKA kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, klabu ya Tanzania Prisons SC ya Mbeya imemsajili kipa Benedict Haule kutoka Azam FC na mshambuliaji Moses Kitandu kutoka Costa Do Sol ya Msumbiji.
  Mkurugenzi wa Ufundi, Kelvin Fredinand amesema Kitandu ni Mtanzania aliyekuwa anacheza Ligi Kuu ya Msumbiji baada ya kuinukia timu ya vijana ya Simba SC na Haule aliyeibukia Mbao FC ya Mwanza alikuwa Azam FC kwa misimu miwili iliyopita.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YASAJILI KIPA WA AZAM, MSHAMBULIAJI WA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top