• HABARI MPYA

  Sunday, August 29, 2021

  CHELSEA PUNGUFU YATOA SARE 1-1 NA LIVERPOOL

  WENYEJI, Liverpool wamelazimishwa sare ya 1-1 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfield.
  Chelsea ilimaliza pungufu leo baada ya Reece James kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 na ushei kwa kuunawa mpira kwenye boksi na kusababisha penalti ambayo Mohamed Salah aliifungia Liverpool.
  James aliikutwa na majanga hayo baada ya kuisaidia Chelsea kupata bao la kuongoza dakika ya 22 kwa kazi yake nzuri kumaliziwa na mfungaji Kai Havertz na sare hiyo inafanya timu zote zifikishe pointi saba baada ya mechi tatu za mwanzo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA PUNGUFU YATOA SARE 1-1 NA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top