• HABARI MPYA

  Thursday, August 12, 2021

  CHELSEA WAIPIGA VILLARREAL NA KUTWAA SUPER CUP ULAYA

  MABINGWA wa Ulaya, Chelsea wametwaa taji la UEFA Super Cup baada ya kuwafunga washindi wa Europa League, Villarreal kwa penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Windsor Park Jijini Belfast, Ireland Kaskazini.
  Chelsea ilitangulia kwa bao la Hakim Ziyech dakika ya 27, kabla ya Gerard Moreno kuisawazishia Villarreal dakika ya 73.
  Kocha Thomas Tuchel akacheza kamari kwa kumuingiza Kepa Arrizabalaga kuchukua nafasi ya kipa Edouard Mendy kwa ajili ya mikwaju ya penalti.
  Na Mspaniola huyo akaenda kuokoa mikwaju miwili kuipa The Blues taji la kwanza la Super Cup tangu 1998.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA WAIPIGA VILLARREAL NA KUTWAA SUPER CUP ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top