• HABARI MPYA

    Saturday, August 28, 2021

    SIMBA QUEENS YASHINDA 4-1 MICHUANO YA CECAFA

    TIMU ya Simba Queens imeanza vyema mechi za kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake ukanda wa Afrika Mashariki baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya PVP FC ya Burundi katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Nyayo Jijini Nairobi, Kenya.
    Mabao ya Simba Queens yamefungwa na beki Mzimbabwe, Danai Bhobho dakika ya 10, winga Mkongo Flavine Mawete Musolo dakika ya 32 na 81 na mshambuliaji mzawa, Aisha Juma Mnunka dakika ya 84.


    Simba Queens itateremka tena dimbani Jumanne kumenyana na Lady Doves WFC ya Uganda, kabla ya kukamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na FAD FC ya Djibouti Ijumaa.
    Bingwa atashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwaka huu nchini Misri, ambayo itahusisha timu nane, nyingine kutoka kanda nyingine barani zitakazogawanywa katika makundi mawili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA QUEENS YASHINDA 4-1 MICHUANO YA CECAFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top