• HABARI MPYA

  Sunday, August 22, 2021

  LUKAKU AFUNGA CHELSEA YAICHAPA ARSENAL 2-0

  WENYEJI, Arsenal wamechapwa 2-0 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa  Emirates Jijini London.

  Pongezi kwa beki wa kimataifa wa England, Reece James aliyemsetia Romelu Lukaku kufunga bao la kwanza dakika ya15, kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 35 akimalizia pasi ya Mason Mount.

  Ni ushindi wa pili mfululizo kwa Chelsea katika mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu baada ya kuichapa 3-0 Crystal Palace na kipigo cha pili mfululizo kwa Arsenal ndani ya mechi mbili za mwanzo za msimu kufuatia kufungwa 2-0 na Brentford.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUKAKU AFUNGA CHELSEA YAICHAPA ARSENAL 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top