• HABARI MPYA

    Wednesday, August 11, 2021

    YANGA SC YAMTAMBULISHA RASMI DICKSON AMBUNDO MCHEZAJI MPYA WA SITA KWENYE KIKOSI CHA MSIMU UJAO

    KLABU ya Yanga imemtambulisha rasmi winga, Dickson Ambundo kama mchezaji wake mpya wa sita kutoka Dodoma Jiji FC.
    Ambundo aliichezea Yanga katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame ikitolewa katika hatua ya makundi baada ya sare mbili na kupoteza mechi moja.
    Anakuwa mchezaji wa sita mpya kutambulishwa baada ya makipa Mrundi, Eric Johola kutoka Aigle Noir ya kwao, Bujumbura na Djigui Diarra kutoka Stade Malien ya kwao, Mali.

    Wengine ni washambuliaji watupu, Wakongo Fiston Mayele kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa na Heritier Makambo kutoka Horoya ya Guinea pamoja na mzawa, Yussuf Athumani kutoka Biashara United ya Mara.
    Yanga inaendelea na utambisho wa wachezaji wake wapya kabla ya Jumapili kupanda ndege kwenda Morocco kuweka kambi hadi itakaporejea kwa ajili ya tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 29.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAMTAMBULISHA RASMI DICKSON AMBUNDO MCHEZAJI MPYA WA SITA KWENYE KIKOSI CHA MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top