• HABARI MPYA

  Friday, August 20, 2021

  TANZANIA PRISONS YAACHA WACHEZAJI 16

  KLABU ya Tanzania Prisons imetangaza kuachana na wachezaji wake 16 waliomaliza mikataba.
  Taarifa ya Prisons imesema kwamba, kati ya hao kuna ambao klabu imefikia uamuzi wa kutowaongeza mikataba ya kuendelea nao msimu ujao na wengine wameamua kuondoka kwenda klabu nyingine.
  Hao ni makipa Jeremiah Kisubi, Andrew Ntala na Prosper Kaini, mabeki Shaban William, Steven Mwaijala, Nico Mwaipaja, Suleiman Mangoma na winga Hamidu Mohamed.


  Wengine ni viungo  Francis Joel, Salumu Bosco, Ramadhan Ibata  na washambuliaji Kassim Mdoe, Stamili Mbonde, Gasper Mwaipasi na Kennedy Kipepe.

  Aidha, uongozi wa Tanzania Prisons upo kwenye mazungumzo na Adili Buha, Shadrack Thomas na Mohamed  Mkopi juu ya mikataba mpya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAACHA WACHEZAJI 16 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top