• HABARI MPYA

    Thursday, August 12, 2021

    YANGA SC YATAMBULISHA WA SABA MPYA, LEO NI BEKI WA KUSHOTO DAVID BRYSON KUTOKA KMC YA KINONDONI

     KLABU ya Yanga imemtambulisha rasmi beki wa kushoto, David Bryson kutoka KMC ya Dar es Salaam kuwa mchezaji wake mpya wa saba kuelekea msimu ujao.
    Bryson anakuwa mchezaji mpya mzawa wa tatu baada ya winga
    winga, Dickson Ambundo kutoka Dodoma Jiji FC ya Dodoma na mshambuliaji Yussuf Athumani kutoka Biashara United ya Mara.
    Wengine wanne ni wa kigeni, makipa Mrundi, Eric Johola kutoka Aigle Noir ya kwao, Bujumbura na Djigui Diarra kutoka Stade Malien ya kwao, Mali na washambuliaji Wakongo Fiston Mayele kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa na Heritier Makambo kutoka Horoya ya Guinea.


    Yanga inaendelea na utambulisho wa wachezaji wake wapya kabla ya Jumapili kupanda ndege kwenda Morocco kuweka kambi ya kujiandaa na msimu hadi itakaporejea kwa ajili ya tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 29.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YATAMBULISHA WA SABA MPYA, LEO NI BEKI WA KUSHOTO DAVID BRYSON KUTOKA KMC YA KINONDONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top