• HABARI MPYA

  Friday, August 27, 2021

  CAS YASOGEZA HADI SEPTEMBA 21 KESI YA MORRISON NA YANGA

   

  MAHAKAMA ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) imesogeza mbele kesi ya klabu ya Yanga dhidi ya wings Mghana, Bernard Morrison hadi Septemba 21, mwaka huu.
  Kwa mujibu wa barua ya CAS kwenda Yanga wanaowakilishwa na Mawakili Alex Mgongolwa na Simon Patrick na kwa Morrison kupitia kwa klabu yake, Simba kesi hiyo itaendelea Septemba 21.
  Yanga wanamlalamikia Morrison kusaini mkataba na Simba akiwa bado ana mkataba na klabu hiyo ya Jangwani.
  Wakati kesi hiyo ikisikilizwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilithibitika Morrison alikuwa ana mkataba na Yanga wakati amassing Simba lakini ilibainika ulikuwa una mapungufu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAS YASOGEZA HADI SEPTEMBA 21 KESI YA MORRISON NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top