• HABARI MPYA

  Monday, August 30, 2021

  DUBE AFUNGA AZAM FC YAICHAPA KABWE 1-0 NDOLA


  TIMU ya Azam FC jana imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Kabwe Worriers bao pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola nchini Zambia.
  Huo ulikuwa mchezo wa pili wa kujipima nguvu kwa Azam FC katika kambi yake ya kujiandaa na msimu mpya Jijini Ndola kufuatia kuchapwa 4-0 na Red Arrows katika mchezo wa kwanza nchini humo Jumatano iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DUBE AFUNGA AZAM FC YAICHAPA KABWE 1-0 NDOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top