• HABARI MPYA

  Monday, August 09, 2021

  YANGA SC YAWATEMA MAKIPA WOTE TEGEMEO WA MSIMU ULIOPITA, MKENYA FAROUK SHIKALO NA MZAWA METACHA MNATA


  KLABU ya Yanga imeachana na makipa wake wawili, Mkenya Farouk Shikalo na mzawa, Metacha Mnata baada ya wote kuitumikia timu kwa misimu miwili.
  Wote wawili walisajiliwa baada ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 nchini Misri katika michuano ambayo Kenya na Tanzania zilipangwa kundi moja, C na walikuwa makipa wa pili Taifa Stars na Harambee Stars.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAWATEMA MAKIPA WOTE TEGEMEO WA MSIMU ULIOPITA, MKENYA FAROUK SHIKALO NA MZAWA METACHA MNATA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top