• HABARI MPYA

    Sunday, August 22, 2021

    KHALID AUCHO AINGIA KAMBINI YANGA MOROCCO

    HATIMAYE kiungo wa kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho amejiunga na klabu yake mpya, Yanga katika kambi ya kujiandaa na msimu mpya Jijini Marrakech nchini Morocco.
    Aucho aliyesajiliwa kutoka Misr Lel Makkasa SC amewasili Marrakech mapema leo na kesho anatarajiwa kuanza mazoezi na wenzake.

    Auchi ni kati ya wachezaji wapya 11 waliosajiliwa Yanga, wengine ni beki wake mpya, Wakongo, mabeki Yannick Bangala Litombo kutoka FAR Rabat ya Morocco, Djuma Shabani AS Vita, winga Jesus Moloko na washambuliaji Fiston Mayele wote kutoka AS Vita ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo (DRC) na Heritier Makambo kutoka Horoya ya Guinea.

    Wengine wapya ni makipa Eric Johola kutoka Aigle Noir ya Burundi, Djigui Diarra kutoka Stade Malien ya kwao, Mali, beki David Bryson kutoka KMC ya Kinondoni, viungo, Khalid Aucho (Misr Lel Makkasa SC), Dickson Ambundo kutoka Dodoma Jiji FC na mshambuliaji Yussuf Athumani kutoka Biashara United.
    Yanga imeweka kambi Jijini Marrakech nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya ambao watauzindua Agosti 29 kwenye tamasha la Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KHALID AUCHO AINGIA KAMBINI YANGA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top