• HABARI MPYA

  Monday, August 16, 2021

  SIMBA SC YATAMBULISHA NYOTA MWINGINE MPYA, SAFARI HII NI MZAWA BEKI ISRAEL PATRICK MWENDA KUTOKA KMC

  KLABU ya Simba imemtambulisha beki wa kulia, Israel Patrick Mwenda kutoka KMC ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
  Huyo anakuwa mchezaji mpya wa sita Simba kuelekea msimu ujao baada ya beki wa kati Mkongo Henoc Inonga Baka kutoka DC Motema Pembe ya kwao, Kinshasa, mawinga Msenegal, Msenegal Papa Ousmane Sakho kutoka Teungueth Rufisque ya kwao, Yussuf Mhilu kutoka Kagera Sugar ya Bukoba, Wamalawi, Peter Banda kutoka Nyasa Big Bullet ya kwao, Blantyre na kiungo Duncan Nyoni kutoka Silver Strikers ya kwao, Lilongwe.
  Kikosi cha Simba SC tayari kipo kambini nchini Morocco kujiandaa na msimu mpya pia na kitarejea kwa ajili ya Tamasha la Simba Day Agosti 28.


  Ikumbukee msimu ujao Simba itawakosa nyota wake wawili walioibeba timu kwa misimu miwili iliyopita, winga wa Msumbiji Luis Miquissone aliyeuzwa Al Ahly ya Misri na kiungo Mzambia, Clatous Chama aliyeuzwa RSB Berkane ya Morocco.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATAMBULISHA NYOTA MWINGINE MPYA, SAFARI HII NI MZAWA BEKI ISRAEL PATRICK MWENDA KUTOKA KMC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top