MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamemtambulisha kiungo wa kimataifa wa Malawi, Duncan Nyoni kutoka klabu ya Silver Strikers ya kwao, Lilongwe kuwa mchezaji wao mpya wa tatu kuelekea msimu ujao.
Nyoni mwenye umri wa miaka 23 tu anakuwa Mmalawi wa pili kusajiliwa Simba SC dirisha hili baada ya winga Peter Banda kutoka Nyasa Big Bullet ya kwao pia, Blantyre.
Wamalawi hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliotambulishwa Simba SC kufika watatu hadi sasa baada ya winga mzawa, Yussuf Mhilu kutoka Kagera Sugar ya Bukoba.

0 comments:
Post a Comment