• HABARI MPYA

  Monday, August 09, 2021

  SIMBA SC YAMREJESHA KIUNGO WAKE KIPENZI CHA MASHABIKI JONAS MKUDE BAADA YA KUTUMIKIA ADHABU YA KUSIMAMISHWA TAKRIBAN MIEZI MIWILI

   KIUNGO Jonas Gerald Mkude amerejeshwa kikosini Simba SC baada ya kusimamishwa kwa takriban miezi miwili kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.
  Baada ya kukosa mechi za mwishoni mwa msimu, Simba ikitwaa mataji yote nchini, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka nchini (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Mkude ataingia kwenye kambi ya kujiandaa na msimu mpya.
  Ikumbukwe Mkude alituhumiwa kwa makosa yanayojirudia na utoro na kuchelewa kambini na Kamati ya Nidhamu ya klabu chini ya Mwenyekiti, Kamanda Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Alhaj Suleiman Kova ikashauri akapimwe ili kujua tatizo linalomsumbua hadi kurudia makosa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMREJESHA KIUNGO WAKE KIPENZI CHA MASHABIKI JONAS MKUDE BAADA YA KUTUMIKIA ADHABU YA KUSIMAMISHWA TAKRIBAN MIEZI MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top