• HABARI MPYA

  Friday, August 27, 2021

  CRISTIANO RONALDO KUREJEA MAN UNITED

  NYOTA Mreno, Cristiano Ronaldo atarejea Manchester United kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Juventus ya Italia.
  Manchester United imethibitisha kurejea kwa mchezaji huyo kwa ada ya Pauni MIlioni 21.4 ambayo Juventus waliitaka kutoka kwa mahasimu, Manchester City na Ronaldo atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 480,000 kwa wiki.
  Ronaldo mwenye umri wa miaka 36, awali alijiunga na United mwaka 2003 akitokea Sporting CP ya kwao, Ureno na akahudumu hadi mwaka 2009 alipotimkia Real Madrid ambako alicheza kwa mafanikio makubwa hadi mwaka 2018 alipohamia Juventus.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CRISTIANO RONALDO KUREJEA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top