• HABARI MPYA

    Thursday, August 13, 2020

    AZAM FC YASAJILI BEKI WA MBAO FC, EMMANUEL CHARLES KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Azam FC imeingia mkataba wa miaka miwili na beki wa kushoto, Emmanuel Charles, kutoka Mbao FC ya Mwanza iliyoshuka Daraja kama mchezaji huru.
    Charles usajili wake ni sehemu ya kuongeza nguvu katika eneo la ulinzi la Azam FC, likiwa ni pendekezo la benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.
    Beki huyo alikuwa na kiwango bora akiwa na Mbao msimu uliopita, akifanikiwa kutengeneza mabao matatu na kufunga mawili.
    Huo ni usajili wa sita kwenye kikosi cha Azam FC kuelekea msimu ujao, wengine wakiwa ni kipa David Kissu, Awesu Awesu, Ally Niyonzima, Ismail Aziz na Ayoub Lyanga.
    Zoezi la usajili litafungwa na kikosi hicho kwa kumalizia nafasi mbili za wachezaji wa kigeni, wanaotarajiwa kutua nchini hivi karibuni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI BEKI WA MBAO FC, EMMANUEL CHARLES KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top