• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 25, 2020

  AZAM FC YAKAMILISHA USAJILI WAKE KWA KUMNASA MSHAMBULIAJI MCAMEROON KUTOKA FORTUNA DU MFOU YA KWAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imefunga rasmi usajili wake wa msimu ujao, kwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon, Alain Thierry Akono Akono.
  Akono anajiunga na timu hiyo inayomilikiwa na Alhaj Shekh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kama mchezaji huru kufuatia kumaliza mkataba wake Fortuna Du Mfou ya kwao.
  Akono tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo tangu wikiendi iliyopita baada ya kufuzu vipimo vya afya.

  Alain Thierry Akono Akono ajiunga na Azam FC kutoka Fortuna Du Mfou ya Cameroom

  Mshambuliaji huyo amekuwa tegemeo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), anakuja Azam FC kuongeza nguvu katika eneo hilo.
  Wakati huo huo: Nahodha wa Azam FC, Aggrey Morris, amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

  Nahodha Aggrey Morris amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja Azam FC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAKAMILISHA USAJILI WAKE KWA KUMNASA MSHAMBULIAJI MCAMEROON KUTOKA FORTUNA DU MFOU YA KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top